Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba
OFISI INAYOHUSIKA
Ofisi ya Rais - Utumishi wa Umma

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Sekretarieti ya Ajira ni chombo ambacho kimekuwa kiungo muhimu kati ya waombaji wa fursa za ajira na waajiri mbalimbali nchini tangu kuanzishwa kwake miaka minne iliyopita.

Waombaji wa fursa za ajira katika Utumishi wa umma zinazotangazwa kupitia Sekretarieti ya Ajira wanapaswa kuzingatia mambo muhimu yafuatayo.

Masharti ya Kufuata katika Maombi ya kazi Serikalini.

  • Mwombaji wa fursa za ajira anapaswa kutembelea tovuti ya Sekretarieti ya ajira mara kwa mara ambayo ni www.ajira,go.tz. Tovuti hii ndiyo hutumika kutoa matangazo mbalimbali ya kazi
  • Waombaji wote wanapaswa kuwa Raia wa Tanzania.
  • Mwombaji anapaswa kuambatanisha  cheti cha kuzaliwa.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingiliakatika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi zakazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji wanapaswa kuambatanisha maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V).
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma kama kidato cha nne, sita, chuo na bodi mbalimbali za kitaaluma
  • Umri usiozidi miaka 45.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

Zingatia:

Pamoja na njia hiyo ya utumaji wa maombi ya kazi Sekretarieti ya ajira upo katika hatua ya kuanza utumaji wa maombi ya kazi kwa njia ya mtandao ( e-application).

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 25-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page