Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata Leseni
OFISI INAYOHUSIKA
Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Utangazaji ni utawanyaji wa taarifa za redio na video kwa hadhira ya mbali iliyosambaa kupitia njia yoyote ya mawasiliano na umma ya redio au picha, lakini ni ile inayohusu mawimbi ya umeme na sumaku (mawimbi ya redio) kwa hiyo, leseni ya utangazaji ni aina ya leseni ya spectra inayotoa idhini ya leseni ya kutumia sehemu ya spectra ya masafa ya redio/ TV katika eneo fulani la kijiografia kwa madhumuni ya utangazaji.

Masharti na Kanuni:

 • Kampuni ni lazima iwe na angalau na hisa 51% zinazomilikiwa na wananchi
 • Mtu haruhusiwi kurusha, kupokea au kuendesha shughuli za utangazaji bila ya leseni ya huduma ya utangazaji
 • Tume itaangalia manufaa ya mmiliki moja juu ya mwingine

Taratibu:

 • Omba kwenye Tume
 • Ambatisha  ombi kwa Tume
 • Wasilisha ada iliyoelezwa kwa Tume  (Hairudishwi)
 • Mpango wa mtandao na programu ya mafunzo yanayohusisha wafanyakazi wa nchini
 • Uthibitisho wa uwezo wa fedha za kuendeshea huduma ya utangazaji
 • Toa taarifa  kwa Tume kadiri itakavyoonekana inafaa
 • Tume itachapisha notisi kwenye gazeti la serikali/ magazeti ya Tanzania kuhusu utoaji wa leseni
 • Katika muda wa siku 14 za kuchapisha notisi, mtu yoyote anaruhusiwa kuweka pingamizi ya utolewaji wa leseni
 • Notisi ya uamuzi itachapishwa pia kwenye Gazeti la serikali na magazeti mengine yoyote
 • Wakati Tume itakapoamua kutoa maombi ya leseni, itaambatisha masharti ya leseni.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 19-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page