Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba
OFISI INAYOHUSIKA
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Umeme ni aina ya nishati inayotumiwa katika maisha ya kila siku kwa kuwashia taa, kuchemshia maji na kuendeshea mashine, zana na vifaa mbalimbali viwandani, ofisini na nyumbani. Usambazaji umeme nchini Tanzania unadhibitiwa na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO).

Maombi ya Njia ya Umeme na Makadirio

Masharti

i. Mteja anatakiwa kulipa ada ya maombi ya Tsh. 5,000 na kujaza fomu ya maombi ya kupatiwa umeme.

ii. Ambatisha nyaraka zote muhimu: picha moja ya mteja na mchoro wa mfumo wa usambazaji nyaya kwenye nyumba/jengo uliochorwa vizuri na kugongwa mhuri wa mkandarasi wa umeme aliyesajiliwa na kufanya kazi hiyo.   

iii. Wasilisha fomu ya maombi Makao Makuu ya TANESCO, Ofisi ya Mkoa au Wilaya.

iv. Gharama za kuunganisha umeme ni kama ifuatavyo:

  • Mteja wa mjini, gharama ni sh. 320,000.
  • Kuunganishiwa umeme vijijini kwa umbali usiozidi mita 30 bila nguzo ni sh. 177,000.
  • Wateja wa vijijini wanaohitaji umeme wa njia moja na nguzo moja, gharama ni sh. 337,740.
  • Wateja wa mjini kwa kupitia nguzo moja gharama ni sh. 515,618.
  • Wateja wa vijijini wanaojengewa njia moja na nguzo mbili gharama ni Sh. 454,654.
  • Wateja wa mjini wanaojenga njia moja na nguzo mbili gharama ni sh. 696,670.

v. Umeme utaunganishwa kwenye jengo lako.

Taratibu

i. TANESCO itapima njia ya umeme katika kipindi cha siku saba kuanzia tarehe ambayo mteja amerudisha fomu  ya maombi ya njia ya umeme iliyojazwa kwa ukamilifu na viambatisho vyote muhimu.

ii. Iwapo mteja amejaza fomu ya maombi ya njia ya umeme na ametoa viambatisho vyote muhimu (picha ya mteja na mchoro wa mfumo wa umeme katika nyumba/jengo uliogongwa mhuri na mkandarasi wa umeme aliyesajiliwa na kufanya kazi ya kufunga nyaya) mteja atapewa makadirio ya gharama za kazi hiyo.

iii. Katika kipindi cha siku saba za kazi ambapo njia ya umeme haizidi mita 30 kutoka nguzo ya karibu zaidi.

iv. Katika kipindi cha siku kumi za kazi pale ambapo njia ya ziada itatakiwa (isiyozidi mita 100)

v. Siku 14 za kazi ambapo mtandao mpya ni lazima uanzishwe au iwapo umeme unahitajika na wateja wa viwanda na biashara.

Ujenzi wa Njia ya Umeme

Iwapo mteja amelipa gharama zote anazodaiwa na kutimiza majukumu mengine yaliyoelezwa kwenye fomu ya maombi ya njia ya umeme na pale inapofaa, awamu zote  za malipo zimetolewa, ratiba ya kuunganishiwa umeme ifuatayo itatumika:

i. Katika siku 30 za kazi kwa mahali ambapo miundombinu iliyopo inaweza kutumika (kwa umbali usiozidi mita 30 kutoka kwenye nguzo  ya kuunganisha ya karibu zaidi).

ii. Katika siku 60 za kazi pale ambapo njia ya kuunganishia haizidi mita 100 (kama mteja yupo katika umbali wa mita 30 na mita 100 kutoka kwenye nguzo ya karibu ya kuunganishia).

iii. Ndani ya siku 90 za kazi pale ambapo mitandao mipya itabidi ianzishwe au njia ya umeme wa msongo mkubwa inahitajika kwa ajili ya wateja wa viwanda na biashara (kama hakuna mtandao wa karibu wa kumwunganishia mwombaji) 

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 25-01-2017
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page