Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Uasilishaji ni mchakato unaomwezesha mtu kuwa mzazi wa mwingine na kwa kufanya hivyo, unahawilisha haki zote na majukumu, pamoja na ushirikishwaji kutoka kwa wazazi au mzazi wake halisi.  Usajili wa watoto walioasilishwa unatawaliwa na sheria ya uasilishaji (sura ya 335) na sheria za uasilishaji za mahakama.  Taasisi ya Serikali inayosimamia uasilishaji nchini Tanzania ni Idara ya Ustawi wa Jamii.

 Masharti:

 • Wazazi wanaoasilsha ni lazima wawe wakazi wa Tanzania.
 • Mmojawapo wa wazazi wanaosilisha kama ameoa au kuolewa ni lazima awe na umri wa miaka 25 au zaidi.
 • Wazazi ni lazima wawe na umri wa miaka 21 zaidi ya mtoto.
 • Wazazi wajane wanaume hawataweza kuasilisha mtoto wa kike isipokuwa kwa sababu maalumu.
 • Bainisha mtoto/watoto wanaostahili kuasilishwa

 Taratibu:

 • Wasiliana na Ofisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya
 • Jaza fomu ya maombi kwa ukamilifu
 • Ni lazima uwe na maelezo ya mawasiliano ya angalau wadhamini watatu wanaokufahamu kwa angalau miaka mitatu na ndugu/jamaa mmoja.
 • Mchakato wa kutafiti mazingira ya nyumbani utakaokuwa na angalau usaili wa mara nne katika familia, ikiwemo kutembelea makazi ya familia.
 • Peleka maombi kwa kamishna wa ustawi wa jamii kwa uthibitisho
 • Ni lazima ubainishwe na ofisa ustawi wa jamii wa wilaya.
 • Ofisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya atawasiliana na idara ya polisi ili kuthibitisha iwapo mtoto ana ndugu/jama yeyote aliye hai na ridhaa ya familia.
 • Ofisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya itamweka mtoto aliyebainishwa kwa wazazi wanaotarajia kumwasilisha kwa jaili ya kumlea kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu.
 • Anza utaratibu wa kisheria wa kuasilisha na amri ya mahakama, wasiliana na
  mwanasheria mwenye uzoefu (wakili)
 • Andika ombi la kumwasilisha rasmi mtoto wako na pata amri ya mahakama
  kutoka mahakama kuu.
 • Shauriana na wakili wako kupata hati ya uasilishaji kwa ajili ya mtoto wako
  aliyeasilishwa.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 19-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page