Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Home     Sera ya Usalama

Usalama wa Tovuti:
Kwa madhumuni ya usalama wa tovuti na kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwa watumiaji wote, program ya Kompyuta ya tovuti kuu inatumia program za Kompyuta za biashara zinazobainisha mabadiliko ya taarifa, kupakia (kuhawilisha nakala ya faili kutoka Kompyuta moja hadi nyingine), na juhudi zisizoidhinishwa pamoja na kufuatilia msongamano katika matandao.

Ulinzi
Ni marufuku kufikia, yaani kuandika au kusoma data au taarifa kutoka kwenye mfumo Fulani wa Kompyuta bila ya idhini, kuwasilisha au kujaribu ama kuharibu au kushambulia (k.m. kwa kutumia program ya Kompyuta yenye nia ya kuharibu) ukurasa wowote, na matini yaliyomo ndani ya Tovuti kuu.

Matini yaliyomo ndani ya tovuti kuu yana haki ya kukataa au kuodoa kiungo chochote chenye taarifa inayopotosha au madai yoyote yasiyo na uthibitisho, au yenye  nia ya kugongana na lengo kuu la Tovuti Kuu ya Serikali ya Tanzania.

Aidha, Viungo vya tovuti kuu havitapeleka taarifa kwenye tovuti yoyote inayoonyesha chuki, upendeleo, ubaguzi wa rangi, dini au kabila.

Upatikanaji wa Viungo vya Nje:
Tovuti kuu ya Serikali ya Tanzania inaunganisha na tovuti nyingine zilizotayarishwa na kuendeshwa na mashirika/taasisi za Serikali na za binafsi.

Hata hivyo, Tovuti kuu ya Tanzania haiwajibiki na kukosekana kwa tovuti yoyote iliyoelekezwa kuunganishwa.

HATUA ZA KISHERIA
Kwa yeyote atakayeingilia usalama wa tovuti kuu hii, atachukuliwa hatua za kisheria ipasavyo.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2013-07-05 07:34:51

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page