Taarifa za Kina
Tarehe ya Kuzaliwa: 1960-12-22
Mahali pa Kuzaliwa: Ruangwa-Lindi.
Ndoa: Ameoa
Maelezo
Elimu
Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alizaliwa Desemba 22, 1960 Wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi alisoma Stashahada ya Uzamili Elimu katika Chuo Kikuu cha Stockholm 1999,Pia alisoma Shahada yake ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 1994-1998,Alipata elimu ya Kidato cha Sita Mtwara TTC – 1991-1993 na elimu ya Kidato cha nne alihitimu katika Shule ya Sekondari Kigonsera 1977-1980 kwa elimu ya msingi aliipata katika Shule ya Msingi Unacho 1970 – 1977
Kazi
Mhe. Majaliwa alifanya kazi ya ualimu mnamo mwaka 1984-1986, na baadaye alipata kuwa Katibu Wilaya mnamo mwaka 2001 na kisha kuwa Katibu Mkoa mwaka 2001-2006.
Siasa
Mheshimiwa Majaliwa alianza harakati za kisiasa 2010 ambapo alipata ubunge wa Jimbo la Ruangwa Mkoani Lindi na aliteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa miaka mitano, katika Serikali ya Awamu ya Nne iliyomaliza muda wake Novemba 5, 2015.Mhe. Majaliwa aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu Novemba 19, 2015 na kuapishwa rasmi Novemba 20, 2015 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli.