Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Profiles Cheo

Hon. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Utumishi:
2015 - 2016 (Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi)
2016 - 2020 (Waziri wa Mambo ya Ndani)

Taarifa za Kina
Tarehe ya Kuzaliwa: 1975-01-07
Mahali pa Kuzaliwa: Makunda, Iramba - Singida.

Ndoa: AmeoaMaelezo


Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Iramba Magharibi mkoani Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Alizaliwa Januari 7 mwaka 1975 katika kijiji cha Makunda kilichopo wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Elimu.  

Alianza elimu ya Msingi katika shule ya Msingi Makunda Iramba mkoani Singida na kuhitimu mwaka darasa la saba mwaka 1993. Alijiunga na Shule ya Sekondari Iliboru mwaka 1994 na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1997.Kufuatia matokeo yake ya kidato cha nne kuwa mazuri, mwaka 1998 Mhe. Mwigulu aliendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari Mazengo na kuhitimu mwaka 2000.Baada ya Kuhitimu Kidato cha sita alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusomea Shahada ya Kwanza ya Uchumi ambayo aliihitimu mwaka 2004 kisha aliendelea na Masomo ya Shahada ya Uzamili ya Uchumi na kuhitimu mwaka 2006. Mwaka 2002  alijiunga na Chuo cha Uongozi  kwa masomo ya Uongozi na kuhitimu mwaka 2003.

Uzoefu.  

Mara baada ya kuhitimu masomo ya elimu ya juu akiwa Mchumi baada ya kuhitimu alijiunga na Utumishi wa Umma katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kitengo cha Sera za Uchumi akiwa mchumi daraja la kwanza. Mwaka 2001 alichaguliwa kuwa mjumbe wa Vijana wa Wilaya ya Iramba wa Chama cha Mapinduzi na mwaka 2008 akawa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na baadaye alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Mwaka 2010 aliacha Kazi Benki Kuu ya Tanzania na kuingia rasmi kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Iramba Magharibi. Katika uchaguzi huo Mhe. Mwigulu alishinda nafasi hiyo.Pia mwaka 2014-2015 alikuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba.  Aidha, katika Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya nne Mhe. Mwigulu aliitumikia Serikali katika Nafasi ya Naibu Waziri wa Fedha.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                        

 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page