Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Profiles Cheo

Hon. Dr. Ali Mohamed Shein

Utumishi:
2001 - 2005 (Makamu wa Rais wa Tanzania)
2005 - 2010 (Makamu wa Rais wa Tanzania)
2010 - 2015 (Rais wa Zanzibar)
2010 - 2016 (Rais wa Zanzibar)
2016 - 2020 (Rais wa Zanzibar)

Taarifa za Kina
Tarehe ya Kuzaliwa: 1948-03-13
Mahali pa Kuzaliwa: Chokocho, Mkoani District - Pemba,zanzibar.

Ndoa: AmeoaMaelezo


Dk. Ali Mohamed Shein  ni Rais wa awamu ya saba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Alizaliwa tarehe 13 Machi 1948 katika kijiji cha Chokocho mkoani Kusini, Pemba -Zanzibar. Alipata elimu ya  msingi Unguja kuanzia 1956 hadi 1964 katika skuli ya Gulioni Boys Primary School. Mwaka 1965 alianza masomo ya sekondari Lumumba College na kumaliza 1968.

Mwaka 1969 alielekea nchini Urusi kujiunga na Chuo Kikuu cha Taifa Vorenezh State kwa mafunzo ya mwaka mmoja ya kufuzu kujiunga na chuo na baadaye kuchukua mafunzo ya shahada ya kwanza na ya uzamili katika fani ya Biokemia ya Utibabu chuo kikuu cha Odessa State alikohitimu mwaka 1975. Mwaka 1984 Dr. Shein alijiunga na Chuo cha Utibabu cha Newcastle Upon Tyne, Uingereza kwa masomo ya uzamivu na kupewa shahada katikafani ya Biokemia ya Utibabu na Tiba za Umetaboli (Clinical Biochemistry and Metabolic Medicine).

Kati ya 1981 na 1995 alihudhuria mafunzo mbalimbali ya hapa nchini na kimataifa, ikiwa ni pamoja na Huduma za Utiliaji Damu na Uendeshaji wa Benki za Damu yaliyofanyika Stockholm, Sweden (1981), Menejimenti na Uongozi Kutegemeana na Hali, Dar es Salaam (1994) na Upangaji wa Programu za Kudhibiti VVU/UKIMWI kwa nchi zinazoendelea, Chuo Kikuu cha East Anglia, Norwich, U.K. (1995).

Dk. Ali Mohamed Shein alianza kazi kama Karani Wizara ya Elimu, Zanzibar, Mei 1969 na baadaye mwaka huohuo alipewa kazi ya Katibu Mkuu Msaidizi ‘B’ wizara hiyo hiyo hadi Septemba 1969 alipoenda Urusi. Kati ya 1979 na 1984 alikuwa Mkuu wa Idara ya Huduma za Maabara ya Patholojia, Wizara ya Afya Zanzibar. Aliporejea kutoka mafunzo ya uzamivu 1989 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Idara ya Patholojia wizarani hapo. Alikuwa Meneja wa Programu, Mpango wa Kudhibiti UKIMWI Zanzibar ndani ya Wizara ya Afya na mshauri wa Wizara kuhusu Huduma za Biokemia ya Tiba na Utambuzi wa maradhi kati ya 1991 na 1995.

Dk. Shein alianza shughuli za siasa alipojiunga na Afro-Shirazi Youth League (ASPYL) akiwa shuleni na mwaka 1968 alichaguliwa Katibu Mwenezi wa ASPYL, chuo cha Lumumba. Kati ya 1973 na 1975 alikuwa Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa Tanzania,Chuo Kikuu cha Odessa, nchini Urusi. Alikuwa mwanachama wa Afro Shirazi Party na mwanzilishi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya TANU na ASP kuungana Februari 1977.

Oktoba  29, 1995 aliteuliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na kufanywa Naibu Waziri wa Afya, Zanzibar, Novemba 13, 1995. Mwaka 1997 alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM -  NEC. Kutokana na nafasi hiyo aliteuliwa kwenye Kamati Kuu ya CCM 2005.

Alishinda  Kiti cha Uwakilishi cha Mkanyageni katika uchaguzi mkuu wa Novemba 6, 2000 na kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi. Aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba na Utawala Bora, Novemba 22, 2000. Dk. Shein aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Julai 13, 2001 na toka wakati huo amekuwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2005, Shein alikuwa ndiye mgombea-mwenza, hivyo alifanywa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuapishwa 21 Desemba, 2005.

Aligombea nafasi ya Rais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, 2010 na kushinda, hivyo kuapishwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Novemba 3, 2010. Amekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) toka Machi 29, 2011. 

 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page