Industries and Trade

Overview

About the Ministry

The Ministry of Industry and Trade was established under the Government notice GN No. 619A of 30th August 2023 of the Ministers. The Ministry of Industry and Trade is one of the priority sectors in making the country to sustain lower middle and reach a middle income economy by 2025, and considering that the Ministry’s Stratergic Plan for 2021/22-2025/26 has been prepared in accordance with the following: Medium Term Strategic Planning and Budgeting Manual of the United Republic of Tanzania (2007 & 2010); The Tanzania Development Vision (Vision 2025); Five years Development Plan III (FYDP Three); CCM Election Manifesto 2020/25; Sustainable Development Goals; Tanzania Agro Processing Industries Development Flagship 2020 and Sector Policies

About the Ministry

About the Ministry

The Ministry of Industry and Trade was established under the Government notice GN No. 619A of 30th August 2023 of the Ministers. The Ministry of Industry and Trade is one of the priority sectors in making the country to sustain lower middle and reach a middle income economy by 2025, and considering that the Ministry’s Stratergic Plan for 2021/22-2025/26 has been prepared in accordance with the following: Medium Term Strategic Planning and Budgeting Manual of the United Republic of Tanzania (2007 & 2010); The Tanzania Development Vision (Vision 2025); Five years Development Plan III (FYDP Three); CCM Election Manifesto 2020/25; Sustainable Development Goals; Tanzania Agro Processing Industries Development Flagship 2020 and Sector Policies

Majukumu ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2023-2024

i.Kutekeleza Miradi ya Kielelezo ya Magadi Soda Engaruka, Makaa ya Mawe - Mchuchuma na Chuma – Liganga;

Majukumu ya Wizara

Wizara ya Viwanda na Biashara imeundwa kwa mujibu wa Hati idhini GN Namba 619A ya mwaka 2023 na Mgawanyo wa majukumu ya ofisi na kupewa majukumu mahsusi  kama ifuatavyo: -

  1. Kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa sera na mikakati ya sekta za Viwanda na Viwanda;
  2. Kusimamia maendeleo ya Viwanda na Biashara;
  3. Kusimamia maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo (SMEs);
  4. Kuendeleza miundombinu ya viwanda;
  5. Kusimamia miliki bunifu;
  6. Kusimamia masuala ya ushindani wa haki;
  7. Kusimamia vipimo, viwango na ubora;
  8. Kusimamia intelijensia ya masoko na kukuza biashara;
  9. Kukuza mauzo ya bidhaa nje ya nchi;
  10. Kusimamia usajili wa biashara;
  11. Kufanya kazi na Taasisi za kimataifa zinazohusiana na Viwanda na Biashara;
  12. Kuimarisha na kuendeleza ufanisi wa rasilimali watu katika Wizara; na
  13. Kusimamia Idara, Taasisi, Programu na Miradi chini ya Wizara.

 

Sekta ya Viwanda Katika Pato la Taifa

Mchango wa Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kwa mwaka 2021 ulikuwa asilimia 8.0 ikilinganishwa na asilimia 8.4 mwaka 2020, sawa na upungufu wa asilimia 0.4.

Vilevile, kasi ya ukuaji wa Sekta ya Viwanda ilikuwa asilimia 5.1 mwaka 2021 ikilinganishwa na asilimia 4.5 mwaka 2020. Ongezeko hilo la ukuaji lilitokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa baadhi ya bidhaa za viwandani kama vile uzalishaji wa biskuti na tambi uliongezeka kwa asilimia 35.5 kila moja, rangi (asilimia 33.9), nguo (asilimia 23.2), chibuku (asilimia 7.2), dawa za pareto (asilimia 6.5), bati (asilimia 6.1), chuma (asilimia 4.9), kamba za katani (asilimia 4.8), nyavu za uvuvi (asilimia 4.6) na saruji (asilimia 0.5) Kwa upande mwingine, Sekta ya Viwanda imetoa ajira 345,615 mwaka 2021 ikilinganishwa na ajira 370,485 mwaka 2020.

Viwanda vimesambaa nchi nzima na sehemu kubwa ya viwanda hivyo ni vidogo sana ambavyo ni 62,400 sawa na asilimia 77.07, wakati vidogo ni 17,267 sawa na asilimia 21.33, vya kati ni 684 sawa na asilimia 0.84 na vikubwa ni 618 sawa na asilimia 0.76.

Kati ya Viwanda Vikubwa 618 (Vinavyoajiri kuanzia watu 100), Viwanda 41 pekee vinaajiri zaidi ya watu 500.Viwanda vingi vinajishughulisha na uongezaji thamani ya mazao ya kilimo na vinajielekeza katika kutumia malighafi za ndani kuzalisha bidhaa hizo.

Kutokana na usajili wa viwanda chini ya TIC na EPZA, inategemewa kuwa viwanda vipya vikubwa 500 vitajengwa kufikia mwaka  2025 na kufanya idadi ya sasa ya viwanda vikubwa vinavyoajiri wafanyakazi zaidi ya 500 kuongezeka kutoka 41 hadi kufikia 541.

Kongani kubwa ya Viwanda ya Kwala itakuwa na viwanda 200 vikubwa kwa ajili ya kutengeneza nguo, vifaa vya umeme, vifaa vya ujenzi, dawa na aina nyingine. Mradi huo umekwishaanza na awamu ya kwanza itakamilika ifikapo mwaka 2024 na viwanda vitatoa ajira za moja kwa moja 100,000 na zisizo za moja kwa moja 300,000. Aidha, uwekezaji katika eneo hilo unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani Bilioni 3 na unalenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha bidhaa za viwanda katika Soko la Pamoja la Afrika.

Sekta ya Biashara Katika Pato la Taifa

Tanzania ina fursa mbalimbali za masoko ya kuuza mazao na bidhaa inayozalisha. Uwezo wa nchi kuuza nje mazao na bidhaa unaongezeka na hususan uuzaji wa bidhaa zilizoongezwa thamani katika masoko ya ndani, kikanda na kimataifa. 

Mchango wa Sekta ya Biashara katika Pato la Taifa kwa mwaka 2021 ulikuwa asilimia 8.9 ikilinganishwa na asilimia 8.7 mwaka 2020 sawa na ongezeko la asilimia 0.2. Vilevile, Kasi ya Ukuaji wa Sekta ya Biashara ilikuwa asilimia 4.0 mwaka 2021 ikilinganishwa na asilimia 2.1 mwaka 2020. Ongezeko hilo linatokana na kuongezeka kwa bidhaa zilizouzwa 29 zikiwa ni pamoja na bidhaa za kilimo na bidhaa zilizozalishwa viwandani. 

Matumizi ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi umeongezeka na hivyo kuchochea kupunguza uagizaji nje wa baadhi ya bidhaa na malighafi na hivyo kuiwezesha nchi kupunguza matumizi ya fedha za kigeni. Pamoja na kuwepo kwa uagizaji wa bidhaa za mwisho (final products), kumekuwa na ongezeko la uagizaji nje wa bidhaa za kati na za mitaji (intermediate input and capital goods) zinazotokana na mahitaji ya viwanda vinavyowekeza hapa nchini. 

Sekta ya Biashara imewezesha uuzaji nje wa bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani 6,755.6 kwa mwaka 2021 ikilinganishwa na Dola za Marekani 6,371.7 kwa mwaka 2020 sawa na ongezeko la asilimia sita (6) Ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa zisizo asilia hususan bidhaa za viwandani, mazao ya mbogamboga na bidhaa nyinginezo zikijumuisha mahindi na mpunga.


 

Settings