Hii ni Tovuti kuu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyo buniwa kutengenezwa na kuendeshwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao kuwarahisishia wananchi kupata taarifa na huduma za Serikali ya Tanzania kwa njia ya Mtandao.
Lengo Kuu
Lengo kuu la Tovuti kuu ni kuwezesha upataji rahisi na wakuaminika wa taarifa na huduma zinazotolewa na Serikali ya Tanzania kwa wananchi, wafanyabiashara, watumishi, wanafunzi, wageni, watu mbalimbali, wawekezaji na wadau wengine. Tovuti kuu hii imefanya jitihada ya kuwa chanzo kamili, sahihi na cha kuaminika cha taarifa kuhusu Tanzania na sekta zake mbalimbali.
Tovuti kuu ya sasa ni datameta yaani ina data zinazoweza kukuunganisha na tovuti nyingine za Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kupata taarifa za hivi karibuni zaidi.
Matini/Maudhui ya Tovuti kuu hii inasimamiwa na Idara ya Habari (Maelezo) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma pamoja na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Lengo ni kuendelea kuiboresha Tovuti Kuu hii kwa upande wa aina Kiwango cha matini/maudhui, usanifu na teknolojia mara kwa mara.
Miundo ya Makala
Muundo mkuu wa taarifa ndani ya Tovuti kuu ni HTML. Hata hivyo makala za mtindo wa PDF (leni Sheria, Nyaraka, Fomu, Hotuba n.k) zimetolewa ili kubakisha muundo wa asili wa makala na au kuwasaidia watumiaji wataopakua, yaani kuhawilisha mafaili kutoka kwenye kompyuta.
Kufungua makala ya mtindo wa PDF ni lazima uwe na program tumizi ya Adobe Reader 4 au program Sakinishi, yaani inayomwelekeza mtumiaji kwenye kompyuta yako. Itafungua makala moja mwingine inachukua muda mrefu kufungua makala ya PDF. Ikitokea hivyo, tunakushauri uipakue kwanza kwenye kompyuta yako halafu ndiyo uifungue kutoka hapo.
Vidokezo vya namna ya kupakua makala kutoka kwenye kompyuta yako:
Iwapo utatumia Mozilla Firefox kama kivinjari chako
Iwapo utatumia chrome kama kivinjari chako:
Iwapo utatumia Safari kama kivinjari chako
Zingatia:
Kwa ubora zaidi itazamwe kwa skrini ya 1024 x 768 (au zaidi).
Je, unahitaji msaada kwa matatizo uliyoyapata kwenye Tovuti kuu hii?
Iwapo umepata matatizo kuhusu Tovuti Kuu hii, tafadhali tuandikie barua pepe kupitia info@ega.go.tz