Nchini Tanzania, Sekta ya Kilimo ni muhimili wa maendeleo ya uchumi. Sekta hii inachangia kiasi cha nusu ya pato la Taifa, robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na chanzo cha chakula pamoja na utoaji wa fursa za ajira zaidi ya 75% ya Watanzania. Kilimo kina uhusiano na sekta zisizo kuwa za kilimo kupitia uhusiano wa usafishaji kwenda kwenye usindikaji wa mazao ya kilimo, matumizi na uuzaji nchi za nje;Inatoa malighafi kwa viwanda na soko kwa bidhaa zilizotengenezwa. Tanzania inazalisha takribani 97% ya mahitaji yake ya chakula. Uzalishaji wa mazao ya chakula unatofautiana mwaka hadi mwaka kutegemea kiasi cha mvua kilichopatikana.
Maendeleo ya kilimo yamekuwa chini ya Serikali/fedha za umma kwa kipindi kirefu. Hata hivyo marekebisho ya uchumi kwa jumla yamekuwa na yanaendelea kuwa na matokeo ya muhimu kwenye sekta ya kilimo. Marekebisho ya kiuchumi yamesababisha kufunguka sekta hiyo kwa uwekezaji binafsi katika uzalishaji na usindikaji , uagizaji pembejeo za kutoka nchi za nje na usambazaji na masoko ya kilimo. Serikali imebaki na kazi ya usimamizi na usaidizi wa umma na dhima ya uwezeshaji.
Taarifa iliyojumuishwa kwenye sehemu hii itakusaidia mwananchi kuelewa kuhusu upimaji wa udongo na rutuba, uhifadhi, masoko na upangaji wa bei, ulishaji wa mifugo, mbolea na viuatilifu, taratibu bora kwenye kilimo cha kutumia mbolea ya asili, ufugaji wa nondo wa hariri, kilimo cha bustani, ufugaji wa samaki, kilimo cha maua na namna ya kupata mikopo ya kilimo na ruzuku. Kwa taarifa zaidi tembelea Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
i. Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II)
Mpango huu unalenga kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo (mazao, mifugo na uvuvi) kuongeza uzalishaji, biashara na kipato cha mkulima wa hali ya chini ili kuboresha hali ya maisha, usalama wa chakula na lishe na mchango katika Pato la Taifa.
Mkakati wa utekelezaji wa mpango huu ni kuwabadilisha na kuwafanya wakulima wadogo wadogo kulima kibiashara kwa kuimarisha na kuamsha vichochezi vya sekta na kuwawezesha wakulima wadogo kuongeza uzalishaji katika bidhaa lengwa ndani ya mifumo ya uzalishaji endelevu na kuanzisha uhusiano endelevu wa soko kwa ajili ya ushindani wa kibiashara na maendeleo ya mnyororo wa thamani.
ii. AGRI-CONNET
Hii ni programu inayofadhiliwa na Umoja wa nchini za Ulaya inayolenga katika kukuza uchumi, kukuza maendeleo ya sekta binafsi na kutengeneza ajira katika sekta ya kilimo, na kuongeza usalama wa chakula na lishe nchini.https://www.kilimo.go.tz/programmes/view/agri-connect
iii.Building a Better Tommorow
Huduma za ugani ni muhimu sana katika kusaidia kupunguza umaskini vijijini na ushindani wa soko kwa ajili ya kilimo cha biashara katika soko la ndani na soko la kimataifa. Huwawezesha wakulima kuongeza mazao na tija kwa upataji taarifa ya huduma za masoko na huduma nyingine za msaada muhimu kwa maendeleo ya kilimo. Mageuzi ya huduma za ugani za kilimo ni muhimu ili kutoa zana sahihi, maarifa na stadi pamoja na kuhakikisha kuwa wakulima wanafuata Kanuni Bora za Kilimo. Mahitaji ya Taifa ya maofisa ugani ni 15,082 ili waweze kuhudumia wakulima katika kila kata na kijiji kwa kuleta ufanisi na tija. Mpaka sasa wapo maofisa ugani 7,974 ambao ni takribani 50% ya jumla ya mahitaji. Juhudi ziko mbioni kuwafunza na kuwapangia wafanyakazi wanaohitajika
Tasnia ya kilimo cha bustani ina umuhimu mkubwa kwa uchumi wa sekta ya kilimo.
Kwa taarifa zaidi tembelea https://www.kilimo.go.tz/resources/view/mkakati-wa-kuendeleza-horticulture
USIMAMIZI NA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI YA KILIMO
Wizara ya Kilimo kupitia Idara ya Usimamizi na Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Kilimo inatoa huduma mbalimbali kama zifuatavyo:-https://www.kilimo.go.tz/resources/view/usimamizi-na-mipango-ya-matumizi-ya-ardhi-ya-kilimo