Elimu

Elimu

Serikali ya Tanzania  imeanzisha juhudi nyingi za marekebisho ya sera na muundo ili kuimarisha ubora wa elimu na kuhakikisha elimu ya msingi kwa wote ili kuimarisha uhusiano kati ya elimu inayotolewa katika ngazi zote za maendeleo ya uchumi na jamii nchini Tanzania.

Elimu ina athari kubwa na muhimu kwa maendeleo ya kijamii na binadamu hasa katika kufuta ujinga wa kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu, umaskini, uzazi, na afya ya mama na mtoto. Elimu ya Msingi ndicho kiwango cha elimu chenye athari kubwa kwa matokeo ya kijamii. Inachangia takriban asilimia 60 ya jumla ya athari, ambayo inahalalisha zaidi uhalali wa juhudi endelevu kuhakikisha kuwa watoto wote wa Tanzania wanamaliza angalau elimu ya msingi; na Elimu inauhusiano mkubwa na mahitaji ya soko la ajira.

Viwango vya juu vya elimu huwezesha kipato kikubwa. Mshahara wa wafanyakazi wenye elimu ya sekondari ni muhimu zaidi na hivyo kuonyesha kuwa kuna upungufu mkubwa wa watu wenye sifa za elimu ya sekondari. Pia kuna uhusiano mkubwa kati ya mafunzo ya ufundi stadi na ajira ya wahitimu wa vyuo. Kwa jumla mapato ya wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi unalingana vizuri na watu waliojiajiri wenye elimu ya msingi au sekondari.

Sehemu hii inaainisha taarifa kamili zinazohusu huduma za elimu kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu, mitaala ya elimu na jinsi gani wanafunzi wanaweza kupata taarifa za majibu ya mitihani, mikopo ya elimu ya juu, jinsi ya kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali. kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Elimu ya Masafa

Elimu ya Masafa imeshamiri sana nchini Tanzania kwa ushirikishaji mkubwa wa Serikali katika utekelezaji wake. Wizara ya Elimu  na Mafunzo ya Ufundi Stadi imetoa mchango mkubwa katika kusaidia maendeleo ya fursa za elimu ya masafa. Sehemu hii inakupatia maelezo ya kina kuhusu Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Bodi ya Huduma za Maktaba, Tanzania.

Elimu ya Juu

Idara ya Elimu ya Juu ina wajibu wa kuratibu sera na miongozo, kuweka viwango, program, masharti na kuhakikisha elimu ya juu bora, kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) Tanzania. Aidha,Idara ya Elimu ya Juu ina wajibu wa kuratibu taasisi zote za elimu ya juu na wakala zilizoko katika Wizara. Katika sehemu hii, pata maelezo ya kina kuhusu Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSAB), Taasisi za Elimu ya Juu, Msaada wa masomo na Vyuo vikuu.

Mikopo ya Elimu ya Juu

Higher Education Students' Loans Board was established by Act No. 9 of 2004 and became operational in July 2005. The objective of the Board is to assist, on a loan basis, needy students who secure admission in accredited higher learning institutions, but who have no economic power to pay for the costs of their education. The Board is also entrusted with the task of collecting due loans from previous loan beneficiaries in order to have a revolving fund in place so as to make the Board sustainable. Due to increasing numbers of applicants seeking loans and limited funds set aside annually by the Government, the Higher Education Students' Loans Board uses Means Testing System in identifying applicants who deserve to be given loans.

The criteria used to get loans include neediness, academic performance in Form VI examinations or equivalent qualifications and national priority programmes. For in-service students not pursuing health science programmes or education in science and mathematics, other arrangements are in place for them to get loans from their employers or Social Security Schemes.

Financial assistance loaned to students covers the following six items;

  • Meals and Accommodation
  • Books and Stationery Expenses
  • Special Faculty Requirements
  • Field Practical
  • Research Expenses
  • Tuition Fees

In this section you will find online application form, and loan repayment form, visit Higher Education Students Loans Board website for more details. 

Mpangilio