Maji ni muhimu kwa maisha na kudumisha mazingira, na yanatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania. Maji yanagusa nyanja zote za maisha ikiwemo nyumbani, kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda, wanyamapori, nishati, michezo na burudani na shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii. Kwa kuzingatia umuhimu wa maji kwa maisha ya watu, Wizara ina mfumo wa kitaasisi kwa ajili ya huduma ya maji, utaratibu wa mifereji ya maji machafu na usafi / udhibiti wa afya, kwa kutenganisha kati ya maji mijini na mifereji ya maji machafu na huduma za maji vijijini.
Kwa upande mwingine Wizara ina wajibu wa kufuatilia ubora wa vyanzo vya maji na kushiriki kwenye shughuli zinazohusiana na kudhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji unaofanywa na maabara 17 za ubora wa maji na usimamizi wa Rasilimali za maji unaofanywa na mabonde ya Maji Tisa. www.maji.go.tz
Program ya Usambazaji maji mijini ilianzishwa mwaka 1997 kupitia Akaunti Maalum chini ya Sheria ya Hazina na Ukaguzi ya mwaka 1961 kufuatia Sheria ya Miundombinu ya Maji Sura ya 281, Masharti ya Nyongeza ya mwaka 1997 iliyoipa dhamana ya Wizara inayohusika kuanzisha asasi zinazojitegemea zinazoitwa Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka Mijini. Kwa lengo la kuimarisha usambazaji wa huduma ya maji na mfumo wa maji machafu Mijini ambako huduma hiyo imekawilishwa kutokana na ongezeko kubwa la watu na kupanuka kwa kaya isiyowiana na mtandao wa maji.
Katika Sheria ya Miundombinu ya Maji, Sura ya 281 ya mwaka 1997 (marekebisho) ilianzisha Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mikoani isipokuwa Mamlaka ya Maji na Mfumo wa Maji Machafu ya Dar es Salaam (DAWASA) inayosambaza maji Dar es Salaam, Kibaha, na Bagamoyo iliyoanzishwa tarehe 1 Januari, mwaka 1998, Mamlaka nyingine iliyoanzishwa baadaye ni Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka ya Babati, mwaka 2003. Maelezo zaidi bofya HAPA
RUWASA ni ufupisho wa Rural Water Supply and Sanitation Agency. Ni Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini iliyoanzishwa kwa Sheria Na. 5 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya Mwaka 2019. RUWASA imeanza kazi mwezi Julai, 2019. Bofya HAPA kupata maelezo zaidi
Wizara ya Maji kupitia Idara ya Ubora wa Maji ina wajibu wa kufuatilia ubora wa vyanzo vya maji na kushiriki katika shughuli zinazohusu udhibiti wa uchafuzi wa vyanzo vya maji. Idara hiyo ina mtandao wa maabara 17 za ubora wa maji nchini. Maabara hizi zipo Arusha, Bukoba, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Musoma, Singida, Shinyanga, Songea, Sumbawanga , Manyara na Tanga. Idara hiyo pia inafanya uchambuzi wa Kemikali za kutibu maji ili kubaini ubora wake kama unatimiza viwango. Sehemu hii inakupa mawasiliano muhimu ya maabara za maji zilizotajwa hapo juu zilizopo nchini kwa ajili ya kupima ubora wa maji.
Maabara ya Ubora wa Maji bofya HAPA
Wakala ya Kuchimba Visima na Kujenga Mabwawa-(DDCA) ni wakala ya serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala za Serikali Nam. 30 ya mwka 1997. DDCA inafanya kazi chini ya Wizara ya majina ilizinduliwa tarehe 26, Mach, 1999. Wakala hii inatoa huduma za upembuzi wakinifu, usanifu na ujenzi wa mabwawa, usanifu na ujenzi wa mifumo ya usambazaji maji, usanifu na uchimbaji wa visima vya kina kirefu. Pia inatoa ushauri wa kiufundi na ushauri mwingine wowote kwa uendelevu wa mradi.
DDCA ina ofisi 5 za kanda nchini kote, ambazo ni kanda ya mashariki, kanda ya magharibi zenye makao yake makuu Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mwanza na Sumbawanga, kwa mfuatano huo. Kwa taarifa zaidi, tembelea tovuti ya.
Usimamizi wa Rasilimali za Maji unafanywa na Ofisi za Bodi za Maji za Mabonde ambazo kwa Tanzania yako Mabonde Tisa. Maelezo zaidi Bofya HAPA
Majukumu yake ni kusimamia na kufuatilia wingi na ubora wa rasilimali za maji pamoja na usalama wa mabwawa. Vilevile, kukusanya takwimu za kihaidrolojia pamoja na za matumizi ya maji; kuandaa ramani za kihaidrolojia, kuandaa vibali vya matumizi ya maji; ukaguzi wa vyanzo vya maji na kuweka mipango ya utafiti wa vyanzo vya maji pamoja na usimamizi wa mazingira ya vyanzo vya maji na kutoa msaada wa kiufundi na elimu ya uhamasishaji juu ya ujenzi wa visima, uhandisi wa masuala ya maji, usimamizi wa maeneo ya matukio na matumizi sahihi ya vyanzo vya maji. Kwa Maelezo zaidi bofya HAPA
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ni mamlaka inayojiendesha ya udhibiti wa sekta mbalimbali iliyoanzishwa kwa Sheria ya EWURA Sura ya 414-2006 ya sheria za Tanzania na marekebisho yake Sheria ya EWURA - R.E 2006, Marekebisho ya Sheria Na. 16 ya 2007, Marekebisho Sheria namba 13 ya mwaka 2008, marekebisho namba 6 ya mwaka 2019 na marekebisho namba 5 ya mwaka 2022. Kwa maelezo zaidi bofya HAPA