Sera ya Faragha

Tamko hili kuhusu faragha linatumika kwa Tovuti Kuu ya Serikali na vyombo vingine vyoyote vya kisheria vinavyodhibiti, kuhakiki au kutumia taarifa zinazoweza kuchukuliwa kupitia kwenye Tovuti Kuu hii bila ya kutoa taarifa yoyote ya binafsi. Hata hivyo mtumiaji, anakubali kutumia data hiyo kwa mujibu wa tamko hili la Sera.

Tafadhali zingatia kuwa Tovuti kuu hii inaweza kuwa na viungo vya kwenye tovuti nyingine, visivyotawaliwa na tamko hili la faragha.

Iwapo mtumiaji ana maswali au kero zozote kuhusu tamko hili la faragha au faragha ya mtumiaji wakati wa kutumia Tovuti kuu hii, kiungo cha “maoni” kinaweza kutumika au kwa kutotumia barua pepe. Tovuti kuu hii ya Serikali haichukui taarifa zako binafsi unapotembelea tovuti yetu, isipokuwa utakapoamua kutupatia taarifa hizo.

Taarifa Inayochukuliwa
Unapotembelea Tovuti Kuu ya Serikali tunaweza kuhifadhi baadhi ya taarifa zikiwemo anwani ya intaneti unakopatia Tovuti Kuu ya Serikali ya Tanzania, tarehe, muda, anwani ya Intaneti ya tovuti ulikounganishwa kwenye Tovuti Kuu ya Serikali ya Tanzania, jina na maneno ya mafaili uliyotafuta/vinjari; mada ulizobofya kwenye ukurasa. Taarifa inayochukuliwa inatumika kubainishia idadi ya watu waliotumia sehemu mbalimbali za tovuti yetu na kubainisha maeneo yenye matatizo. Aidha, tunatumia taarifa hii kuboresha na kuifanya tovuti kuwa na manufaa zaidi. Tovuti kuu ya Serikali inaweza kutumia taarifa hii pia kwa ajili ya uchambuzi wa utafiti.

Taarifa Binafsi
Taarifa binafsi hatuzichukui kwa madhumuni yoyote zaidi ya kushughulikia maombi yako. Taarifa inayojazwa kwenye fomu ya maoni itatumika tu kujibu ujumbe wako, kusaidia kupata taarifa uliyoomba. Taarifa unayotupatia huwa tunawapatia pia wakala nyingine ya Serikali iwapo swali lako linaihusu wakala hiyo, au vinginevyo kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Mpangilio