The Ministry of Works and Transport is mandated to formulate and monitor implementation of Policies on Works, Construction, Transport and their implementation. The Ministry is also responsible for Roads, Bridges, Ferries and Mechanical Matters, Public Works and Government Buildings; Engineering and Design Works, Material Laboratory, Airports Development; Transport Licensing; Civil Aviation; Surface, Marine, Air and Rail Transportation; Harbours and Ports, Safety and Security of Transport; Meteorology; Performance Improvement and Development of Human Resources under this Ministry; Extra-Ministerial Departments, Parastatal Organisations, Agencies and Projects under this Ministry.
Bodi ya usajili ya wasanifu majengo na wakadiriaji ujenzi ilianzishwa kwa sheria ya wasanifu majengo na wakadiriaji ujenzi (usajili) Na. 16 ya mwaka 1997 iliyobatilishwa na kubadilishwa na sheria Na. 4 ya mwaka 2010. Kuhakikisha kuwa wasanifu majengo na wakadiriaji ujenzi wanatoa huduma za kitaaluma zinazokidhi mahitaji ya watu na mazingira yao kwa:
Pata orodha ya wasanifu majengo na wakadiriaji ujenzi waliosajiliwa, fomu za maombi kwaajili ya kupakua na fomu za usajili kwa njia ya mtandao kwenye sehemu hii. Kwa maelezo zaidi tembeleahttp://www.aqrb.go.tz/
Kutokana na kuzingatia kulinda mazingira ya jengo na kulinda wananchi kwa jumla, ni sharti la kisheria kama ilivyoelekezwa katika fungu 5.5 (1)(d) na 5.34 (5) ya sheria namba 4 ya mwaka 2010 kwamba kampuni za usanifu majengo na ukadiriaji ujenzi zihakikishe kuwa zinasajili miradi yao ya ujenzi katika bodi na kwamba ubao wa kuelezea ujenzi unabandikwa stika yenye nembo ya bodi iliyotolewa na bodi. Kampuni za usanifu majengo na ukadiriaji ujenzi zinatakiwa kuchukua nembo ya bodi inayofaa kubandikwa ubao wa eneo la ujenzi katika kutimiza sharti la sheria la wasanifu majengo na wakadiriaji. Ujenzi (usajili) namba 4 ya mwaka 2010, baada ya kujaza kwa ukamilifu fomu za maombi ya nembo zinazopatikana kwenye tovuti ya bodi.
Tasnia ya ujenzi imekuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi katika historia kutokana na umuhimu wake kwenye kujenga miundo mbinu muhimu kwa shughuli za kiuchumi na kijamii katika upataji wa ukuaji endelevu. Baraza la ujenzi la taifa (NCC) linahimiza na kutoa uongozi na kimkakati kwaajili ya ukuaji, maendeleo na upanuzi wa tasnia ya ujenzi nchini Tanzania kwa kutilia mkazo maendeleo ya uwezo wa wananchi kwaajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii na ushindani katika mazingira ya dunia yanayobadilika. Pia NCC inashauri serikali katika mambo yanayohusu maendeleo ya tasnia ya ujenzi na kutoa mapendekezo na ushauri kwaajili ya utekelezaji wao.
Ili kupata orodha ya huduma zitolewazo na NCC katika sehemu hi ina maelezo zaidi tembeleahttp://www.ncc.go.tz/