Mahakama

Sheria na Taratibu

Udumishaji wa Sheria na Taratibu ni majukumu makuu ya serikali. Kimsingi ni sababu ya kuwepo kwa Dola/Taifa. Pia ni jiwe la msingi la kudumishia sheria na taratibu katika jamii ya kidemokrasia na yenye uhuru na mpango mkuu wa utawala bora na kutetea Utawala wa Sheria, ambayo ni dhima ya Taasisi za Sekta. Kwa mtazamo, utengaji wa mafungu ya Serikali hufanywa kama kipaumbele cha juu zaidi kutosheleza ugharimiaji wa shughuli na utolewaji wa fedha kwa wakati. Kwa hiyo Serikali ilianzisha mchakato wa PER kwa bajeti za Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali, Mahakama, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Polisi na Magereza.Soma zaidi ujue jinsi ya kudumisha sheria na taratibu.

HAKI KUZINGATIWA KWA WAKAZI WA NGORONGORO

Serikali imezingatia vyema suala la Haki za Binadamu kwa wakazi waliokuwa wanaishi Ngorongoro kisha kuamua kuanza kuondoka kwa hiyari yao kuelekea Kijiji Cha Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

Serikali imezingatia vyema haki za binadamu, imewajengea nyumba wananchi walioamua kuhama kwa hiyari, imewapa maeneo yasiyopungua hekari 3 kila mmoja, imewasafirisha wao na mizigo yao na mifugo wanayomiliki, lakini pia Serikali imewalipa fidia. Imekuwa ni muhimu wadau wa Haki za Binadamu kukutana na kujadili suala la Ngorongoro na Loliondo ili kuhakikisha haki za binadamu zinazingatiwa na kujibu hoja zisizo za kweli zinazosambaa kwa haraka katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kwa upande wa Loliondo, Serikali imewapa wananchi zaidi ya asilimia 62 ya eneo la hifadhi ya Loliondo ili kukidhi mahitaji ya wakazi wa sasa na imebakiwa na kiasi cha Kilomita za mraba 1500 kutoka 4000 za awali. Mawasilisho ya wataalam yameonesha umuhimu wa kuhifadhi maeneo ya Loliondo na Ngorongoro kutokana na sababu za kimazingira na Ikolojia.

Mpangilio