The Ministry of Information, Communication and Information Technology was established on 12th september, 2021 by the President of the United of Republic of Tanzania. The Ministry is meant to formulate and monitor implementation of policies on information and communication technologies and, Postal services. It is envisaged to drive the digital transformation agenda in Tanzania amid the global fourth phase of industrial revolution.
The Ministry of Communications and Information Technology in collaboration with the Office of the President-PMO-RALG and the Ministry of Lands, Housing and Housing Development, is implementing the Digital Address and Postcode System (NAPA). The purpose of implementing this Framework is to ensure that every institution or citizen has a Residential Address in his or her home, office or business area.
Serikali inatekeleza Mpango wa Anwani za Makazi na Postikodi ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003 inayoelekeza kuwepo kwa Anwani za Kitaifa zitakazowezesha ufikishaji wa barua, nyaraka, vifurushi na vipeto majumbani na katika ofisi mbalimbali. Aidha, nchi wanachama wa Umoja wa Posta Duniani (Universal Postal Union - UPU) katika Mkutano Mkuu uliofanyika Doha, Qatar mwaka 2012 walikubaliana kuanzisha mfumo bora utakaofikisha barua, nyaraka, vifurushi na vipeto kwa wahusika. Kupata taarifa zaidi bonyeza Mwongozo wa Postikodi
Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi una lengo la kuelekeza na kuwezesha Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali na wadau wa Sekta ya Posta namna ya kutimiza wajibu wao katika kusimamia masuala ya Anwani za Makazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Kwa maelezo zaidi bonyeza Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
Mradi Na. 4280: MRADI WA TANZANIA YA KIDIGITALI (DIGITAL TANZANIA) Katika mwaka 2022/23 Sh. 39,300,000,000 fedha za nje ziliombwa kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali. Katika Hotuba ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 vipaumbele vilivyoainishwa kwenye mradi huu ni: (i) Kujenga kituo kimoja (1) cha kukuza taaluma na ubunifu katika TEHAMA na vituo vidogo vitano (5) kwenye kila Kanda; (ii) Kuwezesha ununuzi, ugavi na ufungaji wa vifaa katika kituo kimoja (1) kikubwa na vituo vidogo vitano (5) vya kukuza taaluma na ubunifu katika TEHAMA; (iii) Kuwezesha ununuzi wa ‘bandwidth’ kwa ajili ya matumizi ya intaneti ya Serikali; (iv)Kusimika mitambo kwa ajili ya kuboresha Kituo cha Taifa cha Kutunzia Data (NIDC); (v) Kukarabati vituo 10 vya Huduma Pamoja; (vi)Kujenga mfumo wa kitaifa utakaorahisisha ukusanyaji wa takwimu za masuala ya TEHAMA; (vii) Kujenga, kupanua na kuboresha miundombinu iliyopo ya intaneti yenye kasi (broadband) inayomilikiwa na Serikali (GovNET) na kuunganisha taasisi 100 kwenye Miundombinu hiyo na kufikisha taasisi 390 zilizounganishwa; (viii) Kutekeleza programu ya uelimishaji umma kuhusu mradi; (ix)Kujenga maabara tatu (3) kwa ajili ya kufufua (refurbishment) vifaa vya TEHAMA katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Mwanza; (x) Kujenga minara ya mawasiliano 150 kwenye Kata 150 ili kuwezesha huduma za mawasiliano nchini; (xi)Kufanya mapitio na kuhuisha Sera, Sheria na Kanuni mbalimbali za TEHAMA; (xii) Kuwajengea uwezo wataalam wa TEHAMA nchini kwa kuwapatia watalaam 200 mafunzo ya muda mfupi na wataalam 10 mafunzo ya muda mrefu; na (xiii) Kufanya tathmini ya kuainisha mahitaji na usanifu wa kujenga mfumo wa kuwezesha biashara mtandao. Hadi kufikia tarehe 31 Disemba, 2022 Wizara ilipokea jumla ya kiasi cha Sh. 10,261,846,606.50 sawa na asilimia 26.11% ya bajeti iliyotengwa kwa ajili ya Mradi tajwa. Shughuli zilizotekelezwa kwa kipindi husika ni kama ifuatavyo: (i) Kufanyika maandalizi ya kupata mtaalam kwa ajili ya upembuzi yakinifu kuhusu Kuanzishwa kwa Taasisi ya TEHAMA na vituo vya Ubunifu wa TEHAMA. Mkataba kati ya Wizara na Mshauri Mwelekezi umesainiwa mwezi Disemba, 2022 na kazi hiyo itakamilika mwezi Aprili, 2023; (ii) Kuhakiki taarifa za anuani za makazi katika Halmashauri 11 ambazo ni Majiji ya Dar es salaam na Mwanza, Manispaa za Ilemela, Ubungo, Temeke, Kinondoni, Kigamboni na Mtwara Mikindani, Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Micheweni na Chakechake; (iii) Kufanyika kwa upembuzi yakinifu kwa ajili ya kufanya mapitio ya sera na sheria zinazosimamia TEHAMA. Taarifa ya awali (Final Inception Report) imewasilishwa na Mshauri Mwelekezi na kazi hiyo inarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2023. (iv) Kufanyika kwa Upembuzi yakinifu kuhusu Utengenezaji wa Mfumo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Taarifa za Takwimu za TEHAMA (NISMIS). Mkataba kati ya Wizara na Mshauri Mwelekezi umesainiwa Novemba, 2022 na ameanza kazi ya kukusanya maoni ya wadau kabla ya kuanza kusanifu mfumo huo, utekelezaji wake utakamilka mwezi Mei, 2023. (v) Kukamilisha Mpango Mkakati wa Mfumo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Taarifa za Takwimu za TEHAMA (NISMIS) na orodha ya viashiria vya TEHAMA. (vi) Kuhuisha ununuzi wa Mkondo wa Mawasiliano ya Serikali (Extension of Government Internet Bandwidith) wenye kasi ya 5GBps kwa kipindi kinchoishia mwezi Februari, 2023 kwa ajili kuongeza ubora wa upatikanaji wa huduma za Kidijitali zinazotolewaa na Serikali. Aidha, taratibu za manunuzi ya Mkondo wa Mawasiliano ya Serikali wenye kasi ya 20 GBps kwa kipindi cha miaka kumi ijayo upo katika hatua ya tathmini ya zabuni na Mkataba unatarajiwa kusainiwa mwezi Februari, 2023. (vii) Kufanyika kwa upembuzi yakinifu wa Teknolojia ya (TV White Space) itakayosaidia kuongeza huduma ya mawasiliano kwa watumiaji wa intaneti kwenye maeneo ya vijijini na pembezoni mwa Nchi. Mshauri Mwelekezi amewasilisha taarifa ya awali ya upembuzi na kazi hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2023. (viii) Kukamilika kwa taratibu za Manunuzi ya vifaa kwa ajili ya upanuzi wa Mkondo wa Mawasiliano ya Serikali (Bandwidith termination Equipment). Vifaa hivyo vinatarajiwa kupokelewa mwezi Juni, 2023 na kuboresha uwezo wa Mkondo wa Mawasiliano ya Serikali. (ix) Kuandaa daftari la huduma za Serikali kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za Serikali kwa wananchi (Government Service Directory). (x) Kutangaza ufadhili wa nafasi za masomo kwa watumishi wa Serikali wa kada ya TEHAMA kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili. Uchambuzi wa watumishi watakaofadhiliwa katika mafunzo hayo unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Januari, 2023 na matokeo kutangazwa baada ya kukamilika kwa zoezi hilo. Watumishi wanatarajiwa kaanza masomo mwishoni mwa Mwezi Februari, 2023; (xi) Kufanyika kwa upembuzi yakinifu kwa ajili ya vituo vya huduma Pamoja utakaosaidia kurahisisha utendaji kazi wa vituo hivyo (Business Process reengeering). Taarifa ya awali (Final Inception Report) imewasilishwa. Kazi hiyo inarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2023. (xii) Kufanya maandalizi ya mpango mkakati wa uchumi wa Kidigitali (Digital Economy Framework 2023-2033) utakaosaidia kuongeza matumizi ya kidijitali kwa huduma zinazotolewa na Serikali pamoja na Sekta binafsi. Rasimu ya mkakati huo inatarajiwa kujadiliwa kweye kikao cha Kamati Kuu Tendaji ya Taifa mwezi Januari, 2023.

Mradi Na. 6226: MRADI WA KUENDELEZA UBUNIFU NA UTENGENEZAJI WA VIFAA VYA TEHAMA Katika mwaka wa Fedha 2022/23 Sh. 3,300,000,000 fedha za ndani zilitengwa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kuendeleza Ubunifu na Utengenezaji wa Vifaa vya TEHAMA. Katika Hotuba ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 vipaumbele vilivyoainishwa kwenye mradi huu ni: (i) Kujenga Kituo cha Kuendeleza Wataalam, tafiti na ubunifu wa TEHAMA na kufanya maandalizi ya ujenzi wa makao makuu ya Tume ya TEHAMA; (ii) Kukiendeleza kituo cha kuendeleza kampuni changa za TEHAMA (ICT startups) cha Dar es Salaam (Soft Centre) na kujenga vituo viwili (2) vya Kanda vya kutengeneza bidhaa za TEHAMA; (iii) Kuanzisha Vituo vya Ubunifu na Atamizi TEHAMA katika Wilaya mbili (2) nchini; (iv)Kutengeneza mfumo jumuishi utakaounganisha usajili na uendelezaji wa wataalam na wabunifu TEHAMA nchini (ICT human capital development system); na (v) Kuwezesha shughuli za ufuatiliaji na tathmini ya Mradi. Hadi kufikia tarehe 31 Disemba, 2022 Wizara ilipokea jumla ya Sh. 500,000,000 sawa na asilimia 15.2 ya bajeti iliyotengwa kwa ajili ya Mradi tajwa. Shughuli zilizotekelezwa kwa kipindi husika ni kama ifuatavyo: - i. Usanifu wa kituo cha ubunifu cha Dar es Salaam umekamilika. Hatua za kusaini mkataba na mkandarasi kwa ajili ya kufanya matengenezo na maboresho ya jengo la TEHAMA ziko katika hatua za ukamilishaji na kituo kinatarajiwa kuanza shughuli zake mwezi Machi 2023. ii. Kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa kuainisha mahitaji ya vifaa vitakavyohitajika kwa ajili ya uundwaji wa bidhaa za TEHAMA hapa nchini. Mahitaji yaliyoainishwa yatatumika kuandaa nyaraka za zabuni itakayotangazwa mwezi Machi, 2023. iii. Majadiliano na viongozi wa Mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya ya kupata maeneo ya kuanzisha vituo yanaendelea. Upembuzi na usanifu wa vituo hivyo utafanyika mara baada ya mazungumzo kukamilika mwezi Februari, 2023. iv. Mfumo wa usajili wa wataalamu wa TEHAMA umekamilika ambapo wataalamu wa TEHAMA kutoka maeneo mbalimbali wanaweza kujisajili kupitia https://iprs.ictc.go.tz/. Aidha, Hatua za ukamilishaji wa maboresho ya mfumo wa usajili wa wabunifu wa TEHAMA unatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2023 ambapo utawezesha kuwa na kanzi data ya wabunifu wote wa TEHAMA (ICT/Digital Innovators) nchini, makampuni ya TEHAMA (ICT Companies), Wawekezaji katika huduma na bidhaa za ubunifu katika TEHAMA (Digital Innovation Investors), Vituo atamizi vya TEHAMA (ICT Incubation Hubs), Vituo vya uendelezaji bunifu za kidijitali (Digital Innovation Accelerators) pamoja na Taasisi za kifedha zinazotoa mitaji kwa wabunifu wa TEHAMA (ICT Innovation Capital Investors). v. Wabunifu na Watengeneza bidhaa za TEHAMA 63 wa kanda ya Dar es Salaam walijengewa uelewa wa namna bora ya kukuza bunifu zao ili ziweze kutoa ajira na kuchangia pato la Taifa. vi. Miongozo ya taasisi ikiwemo rasimu ya viashiria hatarishi vya miradi na uendeshaji wa shughuli za Tume imeandaliwa. Aidha, mafunzo ya vihatarishi kwa watumishi na wasimamizi wa mradi yatatolewa mwezi Machi, 2023. vii. Tume kwa kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu vya Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Kilimo Cha Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) na Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) imesaini Hati ya Maelewano na Chuo cha Turku (UTU) kilichopo Finland kwa ajili ya kuanzisha Kituo cha Resilience Academy hapa nchini. Chuo hiki kitasaidia katika kujenga uwezo na kuongeza ujuzi katika masuala ya TEHAMA hususan sekta ya elimu, tafiti, uendelezaji wa miji, mazingira na uhifadhi wa Data za TEHAMA (Strengthening digital competences of universities in education, research and service provisioning related to geospital data, climate risk information management and resilient future development to improve skills and knowledge base of the African Youth for inclusive, safe and resilient urban development).
Mradi Namba 6567: HABARI KWA UMMA Kiasi cha Sh. 940,000,000 kiliombwa kwa ajili ya kukusanya, kuchakata, kuandaa na kusambaza habari na taarifa kwa wananchi kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa Serikali ikiwemo Sera, Mikakati, Miradi na Programu zinazotekelezwa na Serikali. Katika Hotuba ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 vipaumbele vilivyoainishwa kwenye mradi huu ni: (i) Kukusanya, kuchakata, kuandaa na kusambaza habari na taarifa kwa wananchi kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa shughuli za Serikali ikiwemo Sera, Mikakati, Miradi na Programu zinazotekelezwa na Serikali; na (ii) Kukusanya taarifa za mrejesho kutoka kwa wananchi kwa lengo la kupata maoni ya wananchi katika utekelezaji wa majukumu yake. Hadi kufikia tarehe 31 Disemba, 2022 Wizara ilipokea jumla ya Sh 420,797,259.99/- sawa na asilimia 44.8 ya bajeti iliyotengwa kwa ajili ya Mradi tajwa. Shughuli zilizotekelezwa kwa kipindi husika ni kama ifuatavyo: - (i) Ununuzi wa Magari matatu – aina ya Toyota Landcruiser Prado TXL Manual na Toyota Hilux Double Cabin Pick Up mbili (2) ambapo Sh. 347,628,409.99 zimetumika. Pia kiasi cha Sh. 73,168,850.00/- kwa ajili ya kulipia kifaa cha kurushia matangazo mubashara aina ya Live U. (ii) Vipindi ishirini (20) vya Televisheni vinavyohusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo viliandaliwa na kurushwa TBC1. Vipindi hivi vilihusu Kilimo na Umwagiliaji, Viwanda, Ujenzi, Madini na Upanuzi wa Bandari ya Tanga. (iii) Kuratibu Mikutano ya Taasisi za Serikali kutoa taarifa za utekelezaji kupitia vyombo vya habari. Jumla ya Taasisi 37 ziliratibiwa na kutoa taarifa kwa umma kuhusu utekelezaji wa shughuli zake
Mradi Na. 4234: Mfumo wa Anwani za Makazi: Katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Sh. 40,000,000,000 fedha za ndani zilitengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Mfumo wa Anuani za Makazi. Katika hotuba ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 vipaumbele vilivyoainishwa kwenye mradi huu ni: (i) Kuhakiki miundombinu iliyowekwa wakati wa Operesheni Anwani za Makazi ili kuhakikisha viwango vimezingatiwa ili Mfumo uwe na tija kwa wananchi na kuwa endelevu; (ii) Kuhakiki taarifa zilizokusanywa kwenye operesheni maalum ya utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi; (iii) Kuboresha Kanzidata na Programu Tumizi ya Mfumo; (iv)Kuendelea kuunganisha Mfumo wa Anwani za Makazi na Mifumo mingine ya kutoa huduma muhimu za kijamii; (v) Kutoa elimu kwa umma; makundi maalum ya kijamii kuhusu manufaa na matumizi sahihi ya Mfumo na kujengea uwezo Taasisi za umma na binafsi kutoa huduma kupitia Mfumo; (vi)Kutunga Sheria ndogo za kuwezesha ujenzi na matumizi ya Mfumo, mapitio ya Sheria ya EPOCA na Kanuni zake kuwezesha matumizi ya Mfumo; (vii) Kununua servers mbili (2) kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za Mfumo na vifaa vya kuwezesha matumizi ya Mfumo;
(viii)Kuandaa mwongozo wa kufanya maboresho ya namna mpya ya kufanya biashara kwa kutumia Mfumo; (ix)Kutengeneza Mkakati wa usimamizi, uendeshaji na uendelezaji wa Mfumo; na (x) Kuwezesha ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Mfumo. Hadi kufikia tarehe 31 Disemba, 2022 Wizara ilipokea jumla ya kiasi cha Sh. 7,000,000,000 sawa na asilimia 17.5 ya bajeti iliyotengwa kwa ajili ya Mradi tajwa. Shughuli zilizotekelezwa kwa kipindi husika ni kama ifuatavyo: - (i) Kufanya uhakiki wa taarifa za Anwani za Makazi kwenye Halmashauri 12, ambazo ni Majiji ya Dodoma, Arusha, Mbeya na Tanga, Manispaa za Mjini, Magharibi A, Magharibi B na Moshi; na Halmashauri za Kaskazini A, Kaskazini B, Kusini na Kati; (ii) Kuboresha Mfumo wa Kidijitali wa Anwani za Makazi; (iii) Kuandaa Mapendekezo ya maboresho ya sheria za kusimamia Anuani za Makazi; (iv)Kutoa elimu kwa Umma kuhusu Anwani za Makazi; (v) Kuandaa Muundo wa usimamizi na uendeshaji wa Mfumo wa Anuani za Makazi; (vi)Wizara imefanikiwa kutunga Kanuni ndogo za Anuani za Makazi ambazo zimetumika katika kutekeleza mradi wa Anwani ya Makazi