Kuhusu Wizara
Wizara Wizara ya Viwanda na Biashara imeundwa kwa mujibu wa Hati idhini GN Na. 619A ya tarehe 30 Agosti 2023. Wizara hii inatekeleza majukumu yake ya kimuundo kwa kuzingatia maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Serikali, sambamba na mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kama ilivyoainishwa kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs 2030); Agenda ya Afrika 2063; Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2020; na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22-2025/26.
Pia, katika kuchochea kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea kufanya mapitio ya Sera, Mikakati na Sheria za kisekta ili ziweze kuendana na mahitaji ya sasa. Sera hizo ni pamoja na Sera ya Taifa ya Uhamasishaji Uwekezaji (1996); Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda (SIDP, 1996 - 2020); Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo (2003); Sera ya Masoko ya Mazao ya Kilimo (2003); na Sera ya Taifa ya Biashara (2003). Zoezi hilo linakwenda sambamba na kurejea Sheria na Mikakati ya kisekta ikiwemo Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Ngozi na Bidhaa za Ngozi; Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Pamba, Nguo hadi Mavazi (C2C); Mkakati wa Kuendeleza Zao la Alizeti; Sheria ya Kujilinda dhidi ya Athari za Kibiashara (Trade Remedies Act, 2021); Sheria ya Uwekezaji (1997) na Sheria ya Ushindani (2003).
Aidha, Wizara ipo katika hatua mbalimbali za uandaaji wa Sera mpya katika masuala ya ubora (National Quality Policy); miliki ubunifu (Patent Right Policy); ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati na uwekezaji (Local Content Policy); na masuala ya kumlinda mlaji (National Consumer Protection Policy); na mikakati mipya ikiwemo Mkakati wa Kukuza Mauzo ya Nje (National Export Strategy).

Kutekeleza Miradi ya Kielelezo ya Magadi Soda Engaruka, Makaa ya Mawe - Mchuchuma na Chuma – Liganga;
Wizara ya Viwanda na Biashara imeundwa kwa mujibu wa Hati idhini GN Namba 619A ya mwaka 2023 na Mgawanyo wa majukumu ya ofisi na kupewa majukumu mahsusi kama ifuatavyo:-
Mchango wa Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kwa mwaka 2021 ulikuwa asilimia 8.0 ikilinganishwa na asilimia 8.4 mwaka 2020, sawa na upungufu wa asilimia 0.4.
Vilevile, Kasi ya ukuaji wa Sekta ya Viwanda ilikuwa asilimia 5.1 mwaka 2021 ikilinganishwa na asilimia 4.5 mwaka 2020. Ongezeko hilo la ukuaji lilitokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa baadhi ya bidhaa za viwandani kama vile uzalishaji wa biskuti na tambi uliongezeka kwa asilimia 35.5 kila moja, rangi (asilimia 33.9), nguo (asilimia 23.2), chibuku (asilimia 7.2), dawa za pareto (asilimia 6.5), bati (asilimia 6.1), chuma (asilimia 4.9), kamba za katani (asilimia 4.8), nyavu za uvuvi (asilimia 4.6) na saruji (asilimia 0.5) Kwa upande mwingine, Sekta ya Viwanda imetoa ajira 345,615 mwaka 2021 ikilinganishwa na ajira 370,485 mwaka 2020.
Viwanda vimesambaa nchi nzima na sehemu kubwa ya viwanda hivyo ni vidogo sana ambavyo ni 62,400 sawa na asilimia 77.07, wakati vidogo ni 17,267 sawa na asilimia 21.33, vya kati ni 684 sawa na asilimia 0.84 na vikubwa ni 618 sawa na asilimia 0.76. Kati ya Viwanda Vikubwa 618 (Vinavyoajiri kuanzia watu 100), Viwanda 41 pekee vinaajiri zaidi ya watu 500.Viwanda vingi vinajishughulisha na uongezaji thamani ya mazao ya kilimo na vinajielekeza katika kutumia malighafi za ndani kuzalisha bidhaa hizo.
Kutokana na usajili wa viwanda chini ya TIC na EPZA, inategemewa kuwa viwanda vipya vikubwa 500 vitajengwa kufikia mwaka 2025 na kufanya idadi ya sasa ya viwanda vikubwa vinavyoajiri wafanyakazi zaidi ya 500 kuongezeka kutoka 41 hadi kufikia 541.
Kongani kubwa ya Viwanda ya Kwala itakuwa na viwanda 200 vikubwa kwa ajili ya kutengeneza nguo, vifaa vya umeme, vifaa vya ujenzi, dawa na aina nyingine. Mradi huo umekwishaanza na awamu ya kwanza itakamilika ifikapo mwaka 2024 na viwanda vitatoa ajira za moja kwa moja 100,000 na zisizo za moja kwa moja 300,000. Aidha, uwekezaji katika eneo hilo unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani Bilioni 3 na unalenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha bidhaa za viwanda katika Soko la Pamoja la Afrika.
Tanzania ina fursa mbalimbali za masoko ya kuuza mazao na bidhaa inayozalisha. Uwezo wa nchi kuuza nje mazao na bidhaa unaongezeka na hususan uuzaji wa bidhaa zilizoongezwa thamani katika masoko ya ndani, kikanda na kimataifa.
Mchango wa Sekta ya Biashara katika Pato la Taifa kwa mwaka 2021 ulikuwa asilimia 8.9 ikilinganishwa na asilimia 8.7 mwaka 2020 sawa na ongezeko la asilimia 0.2.
Vilevile, Kasi ya Ukuaji wa Sekta ya Biashara ilikuwa asilimia 4.0 mwaka 2021 ikilinganishwa na asilimia 2.1 mwaka 2020. Ongezeko hilo linatokana na kuongezeka kwa bidhaa zilizouzwa 29 zikiwa ni pamoja na bidhaa za kilimo na bidhaa zilizozalishwa viwandani.
Matumizi ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi umeongezeka na hivyo kuchochea kupunguza uagizaji nje wa baadhi ya bidhaa na malighafi na hivyo kuiwezesha nchi kupunguza matumizi ya fedha za kigeni. Pamoja na kuwepo kwa uagizaji wa bidhaa za mwisho (final products), kumekuwa na ongezeko la uagizaji nje wa bidhaa za kati na za mitaji (intermediate input and capital goods) zinazotokana na mahitaji ya viwanda vinavyowekeza hapa nchini.
Sekta ya Biashara imewezesha uuzaji nje wa bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani 6,755.6 kwa mwaka 2021 ikilinganishwa na Dola za Marekani 6,371.7 kwa mwaka 2020 sawa na ongezeko la asilimia sita (6) Ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa zisizo asilia hususan bidhaa za viwandani, mazao ya mbogamboga na bidhaa nyinginezo zikijumuisha mahindi na mpunga.